Marekani yatakiwa kufanya uchunguzi kuhusu vifo vya raia vilivyosababishwa na mashambulizi yake ya anga
2022-03-11 08:59:00| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema Marekani inapaswa kufanya uchunguzi huru, wa kuaminika na usio na upendeleo kuhusu vifo vya raia vilivyosababishwa na mashambulizi ya anga yaliyofanywa na nchi hiyo, na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.

Msemaji huyo alitoa kauli hiyo jana kwenye mkutano na wanahabari, akisema huu ni wito wa wazi kutoka kwa jumuiya ya kimataifa ambao Marekani inatakiwa kuuitikia kwa makini.

Msemaji huyo amesisitiza kuwa maisha ya kila mtu, bila kujali uraia, kabila, dini au imani, ni sawa na yana thamani kubwa.