Makao mkuu ya eneo linalojitawala la Kurd nchini Iraq yashambuliwa kwa makombora
2022-03-14 08:26:07| CRI

Serikali ya eneo linalojitawala la Kurdish nchini Iraq jana imesema, makao makuu ya eneo hilo, Erbil, lilishambuliwa kwa makombora 12, ambayo yalishambulia eneo karibu na ubalozi wa Marekani uliojengwa karibuni katika eneo hilo, na kusababisha majeraha kwa raia mmoja na baadhi ya majengo kuharibiwa.

Kikosi cha ulinzi wa mapinduzi cha Iran kilitangaza kuwajibika na mashambulizi hayo, na kusema kilirusha makombora dhidi ya maeneo yaliyolengwa ya Israel mjini Erbil.