Chuo cha kijeshi cha Ukraine chashambuliwa
2022-03-14 09:22:17| CRI

Jeshi la Russia limeshambulia Chuo cha Jeshi la Nchi Kavu katika eneo la Lviv magharibi mwa Ukraine kwa makombora jana asubuhi.

Vyombo vya habari vya Ukraine vimesema shambulizi hilo la anga limesababisha vifo vya watu 35 na wengine 134 kujeruhiwa. Chuo hicho kilichoko karibu na mpaka wa Poland, ni kituo muhimu cha mafunzo ya kijeshi cha Jeshi la Ukraine.

Habari nyingine zinasema, msemaji wa ikulu ya Russia Dmitry Peskov amesema, hakuna anayekanusha uwezekano wa mkutano wa moja kwa moja kati ya Rais Vladimir Putin wa Russia na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine, lakini ni lazima kufahamu mada watakazojadili marais hao na zitakuwa na matokeo gani.