Shindano la kwanza la Nyimbo za Kichina la "Sauti ya Madagaska" lafanyika mjini Antananarivo
2022-03-14 08:29:03| cri

Fainali ya Shindano la kwanza la Nyimbo za Kichina la "Sauti ya Madagaska" lilifanyika jumamosi huko Antananarivo, mji mkuu wa Madagascar, ambapo mwanafunzi wa kike wa mwaka wa pili kutoka Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Antananarivo alishinda.

Habari zinasema, shindano hilo lilishirikisha watu zaidi ya mia moja. Balozi wa China nchini Madagascar Bw. Guo Xiaomei na wawakilishi 200 kutoka sekta za kisiasa, biashara na kitaaluma za China na Madagaska walihudhuria shughuli hiyo.