Wizara ya mambo ya nje ya China yaitaka Marekani kutoa maelezo kamili kuhusu maabara zake nchini Ukraine
2022-03-15 08:50:43| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema Marekani inapaswa kutoa maelezo kamili kuhusu shughuli zake za kibaiolojia za kijeshi kote duniani, ikiwemo zile zilizofanyika nchini Ukraine, na kuihimiza Marekani kuacha vitendo vya upande mmoja vya kuzuia uanzishwaji wa mfumo wa ukaguzi wa Mkataba wa Silaha za Kibaiolojia (BWC).

Russia hivi karibuni imetoa taarifa kuhusu shughuli za kibaiolojia za kijeshi zilizofanywa na Marekani nchini Ukraine, na kufichua juu ya “dola ya kijeshi ya kibaiolojia” ya Marekani.

Marekani ni nchi inayofanya shughuli nyingi zaidi za kibaiolojia za kijeshi duniani. Katika miongo ya hivi karibuni, shughuli zake hizo zimeendelea kupanuka, huku data zake zikionesha kuwa Wizara ya Ulinzi ya Marekani imedhibiti mamia ya maabara ya baiolojia katika nchi zaidi ya 30, na utafiti wa kibaiolojia wa kijeshi nchini Ukraine ni kipande kiduchu tu cha barafu kubwa.