Askari 13 wauawa katika shambulizi nchini Burkina Faso
2022-03-15 08:54:17| cri

Jeshi la Burkina Faso limesema, askari 13 wameuawa baada ya kuvamiwa na wapiganaji wasiojulikana katika jimbo la Namentenga jumapili iliyopita.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo imesema, basi moja lilishambuliwa kwa mabomu karibu na mji wa Taparko, Mkoa wa Namentenga na kusababisha vifo na majeraha. Kikosi hicho kilienda eneo la mlipuko kufanya kazi za uokoaji, na kuvamiwa na watu wenye silaha wasiojulikana na kusababisha vifo vya askari 13.

Mpaka sasa, hakuna kundi au mtu binafsi kukiri kuhusika na shambulizi hilo.