Ofisa mwandamizi wa kidiplomasia wa China akutana na mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani
2022-03-15 10:43:00| cri

Mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisiti cha China, ambaye pia ni mkurugenzi wa ofisi ya kamisheni ya mambo ya kidiplomasia ya serikali kuu ya China Bw. Yang Jiechi amekutana na mshauri wa masuala ya usalama wa taifa wa Marekani Bw. Jake Sullivan huko Rome.

Pande mbili zimefanya mawasiliano ya kina, kidhati na kiujenzi kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani na masuala ya kimataifa na kikanda yanayofuatiliwa na pande mbili, huku zikikubali kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi mbili, kuongeza maelewano, kudhibiti migongano, kupanua maoni ya pamoja na kuimarisha ushirikiano, ili kuweka msingi wa kuhimiza uhusiano kati ya nchi mbili kurejea katika njia sahihi ya maendeleoiliyo nzuri na utulivu.

Bw. Yang amesema, kutekeleza makubaliano ya pamoja ni jukumu kuu la uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Rais Xi Jinping wa China amependekeza kuwa China na Marekani zinatakiwa kushikilia kanuni za kuheshimiana, kuishi kwa amani na ushirikiano wa kunufaishana, huku akiweka bayana mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Rais Joe Biden wa Marekani pia alitoa ahadi muhimu ya kutotafuta vita baridi, kutobadilisha mfumo wa China, kutoipinga China ili kuimarisha uhusiano wa muungano, kutounga mkono watu wanaojaribu kuitenganisha Taiwan na China bara, kutokuwa na nia ya kupambana na China.

Bw. Yang ameongeza kuwa China siku zote inachukulia na kushughulikia uhusiano kati ya nchi mbili kwa kufuata kanuni tatu zilizotolewa na rais Xi. Na ameitaka Marekani kutekeleza kihalisi ahadi zilizotolewa na rais Biden.