Russia yaanzisha mchakato wa kujitoa katika Baraza la Ulaya
2022-03-16 10:12:40| cri

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetoa taarifa, ikisema nchi hiyo imeanza mchakato wa kujitoa kwenye Baraza la Ulaya.

Taarifa hiyo inadai kuwa, nchi za NATO na Umoja wa Ulaya zinatumia vibaya Baraza la Ulaya, na kulifanya liwe chombo cha kuipinga Russia, na kukataa mazungumzo yenye usawa. Hata hivyo, imeongeza kuwa Russia itaendelea kuwasiliana na nchi wanachama wa Baraza hilo kuhusu masuala yanayofuatiliwa nao kwa pamoja.

Russia ilijiunga na Baraza la Ulaya mwezi Februari mwaka 1996, kama mwanachama wa 39 wa Baraza hilo.