WSJ: China yaongoza katika mtandao wa 5G, hasa katika viwanda
2022-03-16 08:47:03| CRI

WSJ: China yaongoza katika mtandao wa 5G, hasa katika viwanda_fororder_5G

Gazeti la The Wall Street la Marekani limesema, China inaongoza duniani katika kujenga miundombinu ya mtandao wa 5G, hasa kutumia teknolojia hiyo katika viwanda, migodi ya makaa ya mawe, viwanda vya meli na maghala.

Gazeti hilo limesema, China inaonekana kuongoza katika kutumia mtandao wa 5G wenye uwezo mkubwa katika maeneo mengi ya viwanda, ambao unalenga kutumia teknolojia hiyo kusaidia kujiendesha katika viwanda vinavyohitaji watu wengi na michakato ya hatari ya viwanda, na kutarajia kuinua uwezo wa uzalishaji.