Marais wa Ukraine na Russia huenda wakafanya mazungumzo katika siku kadhaa zijazo
2022-03-17 10:35:34| cri

Shirika la habari linaloendeshwa na serikali ya Ukraine Ukrinform limemnukuu mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak akisema, rais Volodymyr Zelensky wa nchi hiyo huenda akafanya mazungumzo na mwenzake wa Russia Vladimir Putin katika siku kadhaa zijazo.

Bw. Podolyak ambaye pia ni mjumbe wa ujumbe wa Ukraine unaoshughulikia mazumgumzo ya amani na Russia amesema, ni wazi kwamba njia pekee ya kumaliza vita hivyo ni mazungumzo ya moja kwa moja kati ya marais wa nchi hizo mbili, na hii pia ni kazi wanayoshughulikia katika mazungumzo yanayofanyika hivi sasa.

Ofisa huyo amesema, kazi ya kuandaa nyaraka zitakazosainiwa katika mkutano kati ya viongozi wa nchi hizo mbili inaendelea.

Ameongeza kuwa upande wa Ukraine una matarajio makubwa kwamba vita vitaweza kusimamishwa hivi karibuni.