Rais wa Madagascar afanya mabadiliko ya serikali
2022-03-17 07:49:35| cri

Rais wa Madagascar Bw. Andry Rajoelina amefanya mabadiliko ya baraza la mawaziri hapo jana.

Baraza hilo jipya linaloongozwa na waziri mkuu Bw. Ntsay Christian lina wajumbe 30, wakiwemo mawaziri 27, makatibu wawili wa serikali na naibu waziri mmoja.

Serikali hiyo mpya inaundwa na wanaume 21 na wanawake tisa.