Gazeti la Renminribao la China jana Jumatano lilichapisha makala ikisema Marekani inapaswa kutoa maelezo kamili kuhusu shughuli zake za kibaiolojia za kijeshi kote duniani, ikiwemo zile zilizofanyika nchini Ukraine.
Makala hiyo inasema Russia hivi karibuni imetoa taarifa kuhusu shughuli za kibaiolojia za kijeshi zilizofanywa na Marekani nchini Ukraine, na kufichua juu ya “dola ya kijeshi ya kibaiolojia” ya Marekani.
Kwa mujibu wa makala hiyo, Marekani ni nchi inayofanya shughuli nyingi zaidi za kibaiolojia za kijeshi duniani. Katika miongo ya hivi karibuni, shughuli zake hizo zimeendelea kupanuka, huku data zake zikionesha kuwa Wizara ya Ulinzi ya Marekani imedhibiti mamia ya maabara ya baiolojia katika nchi zaidi ya 30, na utafiti wa kibaiolojia wa kijeshi nchini Ukraine ni kipande kiduchu tu cha barafu kubwa.
Makala hiyo inaitaka Marekani kusitisha vitendo vya upande mmoja vya kuzuia uanzishwaji wa mfumo wa ukaguzi wa Mkataba wa Silaha za Kibaiolojia (BWC), kwa kuwa kufuata mkataba sio kupiga kelele, na mamlaka ya sheria ya kimataifa inatakiwa kulindwa.