Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.4 latokea Fukushima, Japan
2022-03-17 08:31:25| CRI

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.4 latokea Fukushima, Japan_fororder_VCG111373583634

Watu 3 wamefariki na wengine 130 kujeruhiwa baada ya tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 7.4 kwa kipimo cha Richter kutokea baharini katika mji wa Soma, mkoa wa Fukushima, Japan, saa 5 na dakika 36 usiku wa tarehe 16 kwa saa za huko.

Shirika la Utangazaji la Japan limesema, baada ya kutokea kwa tetemeko hilo, Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa imetoa tahadhari ya kutokea kwa tsunami katika maeneo ya pwani ya mikoa ya Fukushima na Miyagi.