Zambia yafanya mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Rupiah Banda
2022-03-18 08:08:35| CRI

Serikali ya Zambia jana imefanya mazishi ya kitaifa ya rais wa nne wa nchi hiyo Rupiah Banda, yaliyoongozwa na Rais wa sasa wa nchi hiyo, Hakainde Hichilema, na kuhudhuriwa na viongozi wa nchi kadhaa za Afrika.

Rais Hichilema amesema, kifo cha Banda ni hasara kubwa kwa Zambia, na mchango wake kwa Zambia na bara nzima la Afrika utakumbukwa daima.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesema, marehemu Banda ni mwafrika halisi, alikuwa na uzoefu mkubwa wa uongozi, na anastahili kuigwa na viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika.

Rupiah Banda alifariki dunia usiku wa tarehe 11 mwezi huu nyumbani kwake, akiwa umri wa miaka 85.