Rais Xi Jinping wa China asisitiza juhudi za pamoja za China na Marekani kwa ajili ya amani na utulivu wa dunia
2022-03-18 23:23:09| cri

Rais Xi Jinping wa China amesema China na Marekani sio tu zinatakiwa kuongoza uhusiano wao katika njia sahihi, bali pia kubeba wajibu wa kimataifa na kufanya kazi kwa ajili ya amani na usalama wa dunia . Rais Xi ameyasema hayo ijumaa usiku kwenye mazungumzo kwa njia ya video na Rais Joe Biden wa Marekani, aliyeomba kuongea na Rais Xi.

Rais Xi amebainisha kuwa mabadiliko makubwa mapya yametokea katika mazingira ya kimataifa tangu walipowasiliana mara ya kwanza mwezi Novemba mwaka jana, ambapo mwelekeo uliopo wa amani na maendeleo unakabiliwa na changamoto kubwa, na dunia haina amani wala utulivu. Rais Xi pia amesema Mgogoro wa Ukraine si kitu kinachotakiwa kuwepo . Rais Xi amesisitiza kuwa matukio hayo yanaonyesha kuwa nchi hazipaswi kufikia hatua ya kukutana kwenye medani ya vita, na migogoro na makabiliano hayana faida kwa mtu yeyote, na amani na usalama ni mambo ambayo jumuiya ya kimataifa inapaswa kuthamini. Pia amesema Marekani na China zikiwa ni nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi mbili zinazoongoza kwa uchumi duniani, zinapaswa kuongoza uhusiano kati yao uendelee kwenye njia sahihi, na pia zinatakiwa kubeba wajibu wa kimataifa na kufanya juhudi kwa ajili ya amani na usalamawa dunia.