Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu imemalizika hivi karibuni hapa Beijing. Katika michezo hiyo, jumla ya wanariadha 564 kutoka nchi 46 walishiriki katika michezo ya aina sita. Mashindano ya mwaka huu yalishuhudia ongezeko kubwa la wanariadha walemavu wanawake, ambapo kati ya wanariadha 564 walioshiriki, 138 ni wanawake, ikiwa ni ongezeko kutoka wanawake 133 walioshiriki michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu ya Pyongchang mwaka 2018.
Baadhi ya wanariadha walioshiriki kwenye michezo hiyo wamesema ulemavu sio mwisho wa maisha, bali ni vizuri kubadili mtazamo na mwelekeo wa maisha yako, na kutumia fursa uliyonayo kujiendeleza zaidi. Katika kipindi cha Ukumbi wa Wanawake siku hii ya leo tutaangalia jinsi wanawake wanariadha walemavu walivyojitahidi na kuandika historia katika michezo mbalimbali.