Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian jana amesema, mawaziri wa mambo ya nje kutoka Tanzania, Algeria na Zambia wanatarajiwa kufanya ziara ya siku 4 nchini China kuanzia leo. Wakiwa nchini China, mawaziri hao watakutana na kufanya mazungumzo na mwenzao wa China, Wang Yi.