Marekani yahimizwa kuonesha udhati wake kwa dunia
2022-03-19 20:11:20| cri

Rais Xi Jinping wa China jana alipozungumza na rais Joe Biden wa Marekani amesema, nchi mbili za China na Marekani si kama tu zinapaswa kuongoza uhusiano kati yao kusonga mbele, bali pia zinapaswa kubeba wajibu wa kimataifa, na kufanya jitihada kwa ajili ya amani na usalama wa dunia.

Rais Biden amesisitiza kuwa Marekani haitaki haina nia ya kufanya vita baridi vipya dhidi ya China, haina nia ya kujaribu kubadilisha mfumo wa nchi ya China, haina nia ya kupinga China kwa kupitia kuimarisha uhusiano na nchi washiriki wake, haina ni ya kuunga mkono Taiwan ijitenge na China, na haina nia ya kuzusha mgogoro kati yake na China. Rais Xi amesema anatilia maanani kauli hiyo, na kudhihirisha kuwa sababu ya mvutano kati ya China na Marekani ni kwamba Marekani haijatimiza ahadi zake husika, na kuichukulia China kama adui.

Alipozungumzia suala la Ukraine, rais Xi amesema jambo muhimu zaidi la hivi sasa ni kuendelea na mazungumzo, kuepusha vifo na majeruhi ya raia, kuzuia msukosuko wa kibinadamu, na kusimamisha vita mapema iwezekanavyo. Na jambo muhimu zaidi la muda mrefu ni kwamba nchi kubwa ziheshimiane, kuacha wazo la vita baridi, kutopambana kwa makundi, na kujenga mfumo wa usalama wa dunia nzima na kikanda wenye uwiano, ufanisi na uendelevu zaidi hatua kwa hatua.

Katika mazungumzo hayo, Marekani imesema inapenda kufanya mawasiliano na China ili kuzuia hali isipambe moto. China inataka Marekani ioneshe udhati wake, na kuchukua hatua halisi ili kutimiza ahadi za kisiasa za rais Biden.