Waziri wa Mambo ya Nje wa China afanya mazungumzo na wenzake wa Tanzania na Algeria
2022-03-21 14:10:26| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi amefanya mazungumzo na mwenzake wa Tanzania Liberata Mulamula na wa Algeria Ramtane Lamamra ambao wapo ziarani nchini China.

Akiongea na Mulamula kupitia video, Bw. Wang amesema kuwa China iko tayari kutazama uhusiano wake na Tanzania kwa jicho la kimkakati na wa muda mrefu, na kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kina na Tanzania na kutoa mchango mkubwa katika kuijengea uwezo Afrika wa kujitegemea kimaendeleo. Kwa upande wake Bi. Mulamula, amesema kuwa Tanzania imejitolea kujenga uhusiano wake na China kuwa kigezo kipya cha uhusiano wa Afrika na China.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China afanya mazungumzo na wenzake wa Tanzania na Algeria_fororder_9-1

Akiongea na Lamamra Bw. Wang amesema mbali na baadhi ya nchi kujishughulisha na mashindano ya kijiografia, kuna nchi nyingi kama China na Algeria ambazo zina historia ndefu na zinapenda amani na haki. Ametoa wito kwa nchi hizo kuungana mkono na kuimarisha umoja na uratibu ili kukuza mchakato wa demokrasia katika uhusiano wa kimataifa. Naye Bw. Lamamra amesema Algeria inasifu msimamo wa China kuhusu mzozo wa Ukraine na inaamini kwamba mtazamo wa China unaosimamia haki na uadilifu wa kimataifa, na kuzingatia kuhimiza amani, utulivu na usalama ni sahihi na unatia matumaini.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China afanya mazungumzo na wenzake wa Tanzania na Algeria_fororder_8