Rais wa China atoa maelekezo kwa kazi ya uokoaji kufuatia ajali ya ndege
2022-03-21 20:48:06| cri

Ndege nambari MU5735 ya Shirika la Ndege la Mashariki la China imeanguka leo alasiri, ikibeba abiria 123 pamoja na wafanyakazi 9 wa ndege.

Rais Xi Jinping wa China ametoa maelekezo kwa kazi ya uokoaji, akiagiza kuanzisha mara moja mfumo wa dharura, na kuwaokoa watu kwa nguvu zote.

Pia amesisitiza kuchunguza sababu ya ajali hiyo mapema kadiri iwezavyo, kuimarisha kazi ya kuondoa hatari za usafiri wa ndege za abiria, na kuhakikisha kabisa usalama wa watu.