Siku ya Usingizi Duniani
2022-03-22 09:31:30| Cri

Siku ya Usingizi Duniani ni tukio la kila mwaka, linalokusudiwa kusherehekea usingizi na kutoa wito wa kuchukua hatua kuhusu masuala muhimu yanayohusiana na usingizi, ikiwa ni pamoja na dawa, elimu, masuala ya kijamii na kuendesha gari. Kauli mbiu ya siku ya usingizi duniani kwa mwaka 2022 ni Usingizi bora, Akili timamu, Ulimwengu wa Furaha.

Usingizi ni nguzo ya msingi ya afya, na ubora wa usingizi wako unaweza kuathiri sio tu nishati yako ya kimwili asubuhi lakini afya yako ya akili na kihisia pia. Je, wazazi mnazingatia usingizi wa watoto wako? Wakati watoto wanapokua, licha ya lishe na mazoezi, usingizi wenye ubora wa juu ni muhimu sana. Hivyo leo hii katika kipindi cha ukumbi wa wanawake tutaangalia zaidi suala hili la usingizi kwa upande wa watoto.