Ndege ya abiria iliyokuwa imebeba watu 132 yapata ajali kusini mwa China
2022-03-22 09:49:35| CRI

Ndege ya abiria iliyokuwa imebeba watu 132 yapata ajali kusini mwa China_fororder_4

Ndege ya abiria iliyokuwa imebeba watu 132 imepata ajali jana Jumatatu mchana katika mkoani Guangxi, China.

Kwa mujibu wa idara ya usimamizi wa mambo ya dharura, ndege hiyo ya Boeing 737 ya shirika la ndege la China Eastern iliyoondoka Kunming na kupangwa kuelekea Guangzhou, ilianguka saa 8:38 mchana kwenye eneo la milima karibu na kijiji cha Molang katika kaunti ya Tengxian ya mji wa Wuzhou na kusababisha moto mlimani.

Idara ya Usafiri wa Anga ya China imesema kwenye tovuti yake kwamba ndege hiyo MU5735 ilikuwa na abiria 123 na wafanyakazi tisa, na kueleza kuwa sasa imeanza utaratibu wa dharura wa uokozi na kikosi kazi chake kimefika Wuzhou.

Rais wa China Xi Jinping amepokea kwa mshtuko habari za ajali hiyo na kuamuru kuanzishwa mara moja kwa mwitikio wa dharura, juhudi zote za utafutaji na uokozi pamoja na ufumbuzi sahihi baada ya ajali. Rais Xi pia ametaka kuchukuliwa hatua ili kujua sababu ya ajali na kuimarisha usalama kwenye sekta ya usafiri wa anga ili kuhakikisha usalama wa sekta na maisha ya watu.