Watu wasiopungua 25 wauawa kwenye shambulizi, kaskazini magharibi mwa Nigeria
2022-03-22 09:46:11| CRI

Kamishna wa usalama na mambo ya ndani wa Nigeria Samuel Aruwan jana alisema majambazi walifanya shambulizi Jumapili alfajiri huko Agban Kagoro kwenye eneo la Kaura jimboni Kaduna, kaskazini magharibi mwa Nigeria, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 25, na nyumba takriban 70 kuchomwa moto.

Shambulizi hilo limeibua maandamano jana, huku vijana wakizuia barabara na kuwashambulia watalii, na kuilazimisha serikali ya jimbo hilo kuweka marufuku ya kutoka nje kwa saa 24 kwenye maeneo ya serikali za mitaa za Jema'a na Kaura jimboni humo.

Aruwan ametoa taarifa akisema hatua hizo ni kwa ajili ya kuzifanya idara za usalama ziokoe maisha na mali, na kurejesha sheria na utaratibu kwenye maeneo hayo.