Tanzania kufungua vituo vya kiutamaduni katika nchi za nje
2022-03-22 09:46:58| CRI

Serikali ya Tanzania jana ilitangaza kwamba inapanga kufungua vituo vya kiutamaduni kwenye balozi zake zilizoko nchi za nje duniani, ili kuhimiza utamaduni wa Tanzania.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania Bw. Mohammed Mchengerwa amesema kazi ya kuzindua vituo hivyo itaambatana na upelekaji wa maofisa wa mambo ya utamaduni watakaoendesha vituo hivyo. Ameongeza kuwa wizara yake imewasilisha ombi kwa rais Samia Suluhu Hassan juu ya kuidhinisha maofisa hao wa mambo ya utamaduni.