Marekani yatakiwa kuiletea Ukraine amani badala ya mzozo
2022-03-22 09:52:34| CRI

Marekani yatakiwa kuiletea Ukraine amani badala ya mzozo

Bei ya mafuta duniani imepanda hadi dola 100 kwa pipa ambayo ni ya juu zaidi katika miaka hii minane tangu mzozo kati ya Russia na Ukraine ulipozuka mwishoni mwa mwezi Februari, na kuathiri sekta nyingi katika eneo la Afrika kusini mwa Sahara. Kama mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika na yenye uchumi mkubwa zaidi, Nigeria haijafaidika na mgogoro huo kwa sababu ya uwezo wake mdogo wa kusafisha mafuta. Serikali inatoa ruzuku kwa bei za petroli, lakini mafuta ya dizeli na ndege yanauzwa kwa bei ya soko. Mashirika kadhaa ya ndege nchini humo yalionya mwezi huu kwamba yalilazimika kusitisha safari za ndege kutokana na uhaba wa mafuta ya ndege.

Nchi za Afrika zinanunua ngano na mbolea kwa wingi zaidi kutoka Russia na Ukraine, na mzozo huo na vikwazo vya nchi za Magharibi kwa Russia pia vimeongeza gharama ya uzalishaji wa kilimo barani Afrika, na kuchochea mfumuko wa bei na hatari ya kutokea kwa msukosuko wa usalama wa chakula. Nchini Kenya, gunia la kilo 50 la mbolea ambalo liligharimu shilingi 4,000 (kama dola 35) mwaka jana sasa ni shilingi 6,500 (dola 57), huku bei ikitarajiwa kupanda zaidi msimu wa upandaji unapoanza mwezi huu.
Katika nchi ya kusini mwa Afrika ya Malawi, bei ya mkate na mafuta ya kupikia imepanda kwa wastani wa 50%. "Vita hivi havina uhusiano wowote nasi, si sawa kwetu kulipa bei ya juu namna hii," Fatsani Phiri, mkaguzi wa hesabu aliyenunua mkate katika mji mkuu Lilongwe, alimwambia mwandishi wa habari aliyemhoji, “kila wakati vita vinapotokea mahali fulani duniani, waathirika ndio sisi."
Migogoro ya kijiografia na ushindani mkubwa wa nchi kubwa haipaswi kulipwa na watu wa Afrika, na kwamba kuongezeka kwa vikwazo vya upande mmoja kumesababisha kupasuka kwa mnyororo wa kimataifa wa ugavi na uzalishaji viwandani, ambao umeharibu pakubwa maisha ya nchi za Afrika ambazo hazina uwezo wa kutosha wa uzalishaji. Kama Amaka Anku, mchambuzi wa kampuni ya kutoa ushauri wa hatari ya kisiasa ya Marekani Eurasia Group alivyosema, ikiwa mgogoro huo utaendelea, sio tu baadhi ya nchi za Afrika zinazoagiza kwa wingi mafuta na nafaka, zitaathirika vibaya, zile zenye madeni makubwa pia zitashindwa kupata mikopo wakati wawekezaji wanapunguza nia ya kukopesha. Naye Kristalina Georgieva, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), anasema wazi zaidi, "Vita vya Ukraine vinamaanisha njaa barani Afrika."
Umoja wa Mataifa hivi karibuni ulipitisha mkutano kuhusu azimio la mzozo wa Ukraine, China na nchi nyingi za Afrika, zikiwemo Afrika Kusini na Tanzania, hazikupiga kura. Hali halisi ni kuwa, kutopiga kura kunaonyesha kwamba China na Afrika zote zinajiamulia zenyewe sera zao za kigeni, na zinapinga fikra ya Vita Baridi na makabiliano ya kikundi. Muhimu zaidi ni kuwa, kutopiga kura kunaonyesha mtazamo wa kuwajibika wa China na Afrika wa kupinga matumizi ya nguvu na sio kutumia vikwazo kutatua mzozo wa sasa, kwa sababu mazungumzo ndio suluhisho la msingi. Lakini baadhi ya nchi za Magharibi kwa makusudi hazifanyi hivi. Ama zinaipatia Ukraine silaha kwa ajili ya kupata "fedha za vita" na "kuifanya NATO kuwa na nguvu tena", au kuiwekea Russia vikwazo vikali, na kama gazeti la the Sight la Russia lilivyosema "Ili kuishambulia Russia, Marekani inapanga watu wa dunia wafe kwa njaa."
Hivi karibuni, waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi alifanya mazungumzo na wenzake wa Algeria, Zambia na Tanzania waliofanya ziara nchini China, akitoa maoni yake kuhusu athari za mzozo wa Ukraine kwa Afrika. Alisema kuwa mgogoro wa Ukraine unaenea duniani kote, lakini bara la Afrika haswa halipaswi kusahaulika, halipaswi kuwekwa kando, wala halipaswi kuwa mwathirika. Ni kweli kwamba kadiri hali ya kimataifa inavyozidi kuvurugika, ndivyo sauti za nchi za Afrika zinavyohitajika kusikika. Wakati Afrika inaathiriwa na mzozo huo, China pia itasimama nayo kidete.