Nchi za BRICS zazindua kituo cha chanjo (R&D)
2022-03-23 10:48:32| CRI

Nchi za BRICS zazindua kituo cha chanjo (R&D)_fororder_8

Hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Utafiti na Uendelezaji wa Chanjo cha BRICS (R&D) ilifanyika jana Jumanne mtandaoni.

Wakati wa hafla hiyo, waziri wa Sayansi na Teknolojia wa China Bw. Wang Zhigang amesema kuwa China itashirikiana na nchi nyingine za BRICS kutumia uzinduzi wa kituo hicho kama fursa ya kukuza mabadilishano na ushirikiano katika utafiti na upimaji wa chanjo. Ameongeza kuwa China itashirikiana na nchi hizo kuanzisha viwanda pamoja, kutoa idhini ya uzalishaji na kutambua vigezo vya kila upande , ili kuimarisha ulinzi dhidi ya COVID-19 na kutoa matumaini na imani ya kufufua uchumi wa dunia.

Katika hafla hiyo, nchi tano za BRICS zilipendekeza kwa pamoja mpango wa kuimarisha ushirikiano wa chanjo ili kuhakikisha upatikanaji na uwezo wa kumudu chanjo katika nchi zinazoendelea kupitia usambazaji wao wa usawa kama bidhaa za umma za kimataifa.

Mpango huo pia unalenga kuimarisha uwezo wa nchi za BRICS kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na kukabiliana na matukio ya afya ya umma.