China yaitaka Marekani kutengua vikwazo dhidi ya maafisa wa China
2022-03-23 10:45:52| CRI

China yaitaka Marekani kutengua vikwazo dhidi ya maafisa wa China_fororder_7

China jana imeitaka Marekani kutengua vikwazo mara moja walivyowawekea maafisa wa China kwa kile wanachokiita ukiukwaji wa haki za binadamu, na kuonya kuwa vinginevyo China nayo itaijibu Marekani kwa kuiwekea vikwazo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje Wang Wenbin amesema taarifa ya Marekani imejaa itikadi ya upendeleo na uwongo wa kisiasa, kuidhalilisha China na kuwakandamiza maafisa wa China bila sababu. Amefafanua kuwa ilichofanya Marekani kinakwenda kinyume na sheria na kanuni za kimataifa, na kuingilia vibaya mambo ya ndani ya China, hivyo China inapinga vikali jambo hili.

Bw. Wang ameongeza kuwa mkiukaji mkubwa wa haki za binadamu duniani ni Marekani yenyewe, na kwamba inapaswa kutubu kwa kuwaua Wamarekani wa asili na kupunguza idadi yao kutoka milioni 5 ya karne ya 15 hadi laki 2.5 mwanzoni mwa karne ya 20.