Darasa la pili la moja kwa moja laendeshwa kwenye kituo cha anga za juu cha China
2022-03-24 10:52:35| CRI

Darasa la pili la moja kwa moja laendeshwa kwenye kituo cha anga za juu cha China_fororder_课

Darasa la pili la moja kwa moja kutoka kwenye kituo cha anga za juu cha China limeendeshwa Jumatano mchana kwa wanafunzi duniani na wanaanga Zhai Zhigang, Wang Yaping na Ye Guangfu wa chombo cha Shenzhou-13.

Darasa lilianza saa 9:40 alasiri kwa saa za Beijing na kuhudhuriwa na wanafunzi waliopangwa kwenye madarasa matatu nchini China. Darasa kuu liliwekwa katika Makumbusho ya Sayansi na Teknolojia ya China, na mengine yaliwekwa Lhasa katika mkoa unaojiendesha wa Tibet na Urumqi, mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur.

Kwa mujibu wa Idara ya Anga za Juu ya China, muhadhara huo uliotolewa kwa dakika 45 ulihusu utambulisho wa vifaa vya sayansi ya anga ya juu na kipindi cha Maswali na Majibu ya papo kwa papo na wanafunzi kupitia video ambapo mwanaanga Wang akisaidiwa na wanaanga wengine wawili pia walifanya majaribio kadhaa ya kisayansi.

Disemba 9, 2021, watatu hao walitoa muhadhara wa kwanza wa moja kwa moja kutoka kituo cha anga za juu cha China, na kuwaonesha wanafunzi maeneo yao wanayokaa na kufanya kazi.