Tanzania kunufaika na uchunguzi wa Kifua Kikuu na magonjwa sugu ya mapafu
2022-03-25 10:07:34| CRI

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Tanzania inatarajiwa kuboresha uchunguzi na matibabu ya Kifua Kikuu na magonjwa mengine sugu ya mapafu yakiwemo saratani ya mapafu, baada ya mpango mpya wa kuzuia na kutoa huduma ya Kifua Kikuu katika jamii kwa kuchunguza magonjwa sugu ya mapafu kuonesha matokeo mazuri katika mkoa wa Tanga.

Taarifa iliyotolewa na WHO jijini Dar es Salaam imesema Shirika hilo likishirikiana na Wizara ya Afya wamesaidia mradi wa majaribio katika mkoa wa Tanga kama sehemu ya juhudi za dunia za kujumuisha shughuli za Kifua Kikuu na magonjwa sugu ya mapafu katika jamii kwa ajili ya kuchunguzwa mapema.

Taarifa hiyo iliyotolewa ili kuadhimisha Siku ya Kifua Kikuu Duniani, imesema moja ya matarajio muhimu ya mradi huo wa majaribio ni kuongeza ufanisi wa upimaji wa magonjwa sugu ya mapafu ambayo awali yalitambuliwa kimakosa.