Kim Jong Un atoa amri ya kurusha kwa majaribio aina mpya ya kombora lenye masafa ya kusafiri kati ya mabara Hwasongpho-17
2022-03-25 10:05:43| CRI

Kim Jong Un atoa amri ya kurusha kwa majaribio aina mpya ya kombora lenye masafa ya kusafiri kati ya mabara Hwasongpho-17_fororder_5

Shirika la habari la Korea (KCNA) limeripoti kuwa majaribio ya kurusha aina mpya ya kombora lenye masafa ya kusafiri kati ya mabara (ICMB) Hwasongpho-17 nchini Korea Kaskazini yalifanyika jana Alhamis chini ya maelekezo ya rais Kim Jong Un.

Kwa mujibu wa KCNA, Kim Jong Un naye pia alikwenda kwenye uwanja wa kufanya majaribio ya urushaji wa aina hiyo mpya ya kombora na kuongoza mchakato mzima.