Jordan, Rwanda, DRC, Msumbiji, na Tanzania zaapa kupambana na ugaidi
2022-03-25 10:09:27| CRI

Taarifa iliyotolewa na Mahakama ya Kifalme ya Hashemite imesema kuwa Mfalme Abdullah II wa Jordan alishiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa kupambana na misimamo mikali na ugaidi wa Aqaba na marais wa Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Msumbiji, na Waziri Mkuu wa Tanzania uliofanyika katika mji wa pwani wa Jordan Aqaba.

Katika duru mpya ya mkutano huo, washiriki wamesisitiza umuhimu wa kuendelea kukabiliana na vitisho vya makundi ya kigaidi na yenye misimamo mikali. Pia wamehimiza ushirikiano unaoendelea na kubadilishana wataalamu kuzuia upanuzi wa makundi ya kigaidi katika maeneo mapya.

Taarifa hiyo imesema wawakilishi wa mashirika ya kijeshi na usalama kutoka nchi za Afrika, Ulaya, Asia Mashariki na Amerika Kusini pia walijiunga na mkutano huo.