China yakaribisha njia yoyote inayoweza kupunguza msukosuko wa kibinadamu nchini Ukraine
2022-03-25 10:13:29| CRI

China yakaribisha njia yoyote inayoweza kupunguza msukosuko wa kibinadamu nchini Ukraine_fororder_3

Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Zhang Jun jana akihudhuria mkutano wa dharura juu ya suala la Ukraine kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa alisema, China inakaribisha pendekezo na njia yoyote inayoweza kusaidia kupunguza na kutatua msukosuko wa kibinadamu nchini Ukraine.

Zhang amesema madhumuni ya kimsingi ya China ni kuhimiza jumuiya ya kimataifa na Umoja wa Mataifa zitilie maanani hali ya kibinadamu nchini Ukraine. China inatoa wito kwa pande husika kuimarisha uratibu juu ya suala la kibinadamu, kulinda usalama wa raia hasa wa wanawake na watoto, na kutoa wepesi wa kuwahamisha watu na operesheni za msaada wa kibinadamu.

Ameongeza kuwa katika kutatua suala la kibinadamu nchini Ukraine, inapaswa kufuata kwa makini kanuni za kibinadamu, kutopendelea upande wowote, na haki zilizotolewa na Azimio 46/182 la Baraza Kuu la UM, ili kuzuia kulifanya suala la kibinadamu liwe la kisiasa.