Xi aomboleza wahanga wa ajali ya ndege ya China
2022-03-28 16:30:16| cri

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ilifanya mkutano mchana wa Machi 28, ili kutathmini kazi za hivi karibuni.

Kutokana na mapendekezo ya Xi Jinping, ambaye ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, ambaye pia ni Rais wa Nchi, na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, Mwanzoni mwa mkutano huo, wajumbe wote wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC waliohudhuria mkutano huo walisimama na kukaa kimya kwa muda ili kuwaomboleza watu waliofariki katika ajali ya ndege ya MU5735 ya Shirika la Ndege la China Eastern iliyotokea Machi 21.