Wahanga wa ajali ya ndege ya China waombolezwa
2022-03-28 08:48:35| CRI

Shughuli ya maombolezo ya vifo vya watu 132 vilivyosababishwa na ajali ya ndege ya Shirika la ndege la China Eastern, ilifanyika jana kwenye eneo la ajali mkoani Guangxi kusini mwa China, ambapo wafanyakazi kutoka makao makuu ya idara ya taifa ya uokoaji walikaa kimya kwa muda wa dakika tatu kwa kuwaomboleza wahanga. Mjumbe wa taifa wa China Bw. Wang Yong alishiriki kwenye shughuli hiyo.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737-800 iliyokuwa inasafiri kutoka mji wa Kunming kuelekea Guangzhou, ilianguka Machi 21 na kusababisha vifo vya watu wote 132 waliokuwa kwenye ndege hiyo.

Mkuu wa idara ya zimamoto ya mji wa Guilin anayeongoza kazi ya usakaji Bw. Li Shaolin, amesema wamefanya kazi kwenye eneo la ajali na kwenye milima ya karibu kwa siku kadhaa sasa, wakitarajia miujiza. Maelfu ya watu pia wanashiriki kwenye kazi hiyo, wakisaidiwa na droni na vifaa vingine.