Somalia yavunja jaribio la shambulizi la kigaidi na kuwaua wapiganaji 12 wa Al-Shabaab
2022-03-28 08:51:07| CRI

Vikosi vya usalama vya Somalia jana jumapili vilivunja jaribio la shambulizi dhidi ya kituo cha kijeshi katika jimbo la kaskazini mashariki la Puntland, na kuwaua wapiganaji 12 wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab.

Kwa mujibu wa duru za kijeshi nchini Somalia, askari watatu wa Vikosi vya Usalama vya Puntland (PSF) waliuawa kwenye shambulizi hilo karibu na kijiji cha Af-Urur mapema Jumapili asubuhi.

Hivi karibuni kundi la Al-Shabaab limekuwa likifanya mashambulizi dhidi ya maofisa wa serikali, wajumbe wa tume ya uchaguzi na raia wa kawaida kote nchini Somalia, ili kuzuia mchakato wa uchaguzi unaoendelea.