Namibia kuandaa mashindano ya kwanza ya sanaa za mapigano duniani
2022-03-28 08:50:35| CRI

Namibia itakuwa mwenyeji wa Mashindano ya Sanaa za Mapigano Duniani yatakayofanyika kuanzia Machi 29 hadi Aprili 2 katika hoteli ya Safari mjini Windhoek.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo, Shihan Mangaba amesema kupitia taarifa kuwa mashindano hayo yatashirikisha wanamichezo wapatao 600 kutoka nchi na sehemu 40.

Ofisa huyo amesema, hii ni fursa kubwa kwa vijana wa Namibia, ambao wamekuwa wakisubiri kwa miaka mingi fursa ya kupata mafunzo na kushiriki kwenye mashindano ya kiwango cha juu, na kwamba zamani vijana wa Namibia walitakiwa kwenda Japan au Ulaya kwa gharama kubwa ili kuweza kushiriki kwenye shughuli kama hiyo.