Russia na Ukraine kufanya duru mpya ya mazungumzo ya amani
2022-03-28 09:06:35| CRI

Mkuu wa ujumbe wa mazungumzo wa Russia Bw. Vladimir Medinsky amesema ujumbe wa Russia na Ukraine utafanya duru mpya ya mazungumzo ya ana kwa ana tarehe 29 na 30 mwezi huu.

Kuanzia tarehe 28 Februari, Russia na Ukraine zimefanya duru tatu za mazungumzo ya amani ya ana kwa ana na kufanya majadiliano kwa njia ya mtandao wa intaneti, lakini zimeshindwa kufikia makubaliano.

Duru mpya ya mazungumzo itafanyika baada ya jeshi la Russia siku ya Ijumaa kutangaza kukamilika kwa hatua ya kwanza ya operesheni maalum ya kijeshi ya Russia nchini Ukraine Mjumbe wa Ukraine Bw. David Arakhamia amesema duru hiyo mpya ya mazungumzo yatafanyika nchini Uturuki.