Mashirika ya kijamii ya China yaeleza mafanikio ya ulinzi wa haki za wanawake na watoto
2022-03-29 10:23:58| CRI

Mashirika ya kijamii ya China yameeleza juhudi za China katika ulinzi wa haki za wanawake na watoto katika mkutano wa 49 wa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.

Mashirika hayo yameeleza mchango wa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Beijing katika kuwahimiza wanawake kuwa na haki sawa ya kushiriki kwenye michezo, na kuisisitiza jumuiya ya kimataifa kuweka mazingira bora zaidi kwa ajili ya kuhakikisha usawa wa haki za wanawake.

Shirika la mawasiliano ya kimataifa la China limeeleza hali ya ulinzi wa haki za wanawake mkoani Xinjiang, na kusema mazingira ya maendeleo ya wanawake mkoani Xinjiang yameendelea kuboreshwa na wanawake wengi zaidi wameshiriki kwenye ujenzi wa uchumi na jamii mkoani Xinjiang.