Kiongozi wa Sudan Kusini aahidi kutelekeza makubaliano ya amani licha ya changamoto
2022-03-29 09:18:23| CRI

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amehakikishia nchi yake kwamba atatekeleza makubaliano ya amani ambayo yalimaliza mapigano yaliyodumu kwa miaka licha ya changamoto mbalimbali.

Rais Kiir amesema hayo kwenye mkutano na wanahabari, huku akitoa wito umoja katika utekelezaji wa makubaliano ya amani, na kuihakikishia nchi hiyo kwamba hakuna sababu ya wasiwasi.

Rais Kiir amesema makubaliano hayo ni njia ya kutimiza utulivu na ameahidi kuwa watatekeleza makubaliano hayo.  

Pia amesema utekelezaji kamili wa makubaliano ya amani hauwezi kutimizwa bila mazungumzo endelevu kati ya pande husika, huku akieleza kuwa mara kwa mara pande za makubaliano hayo zinakumbwa na vizuizi vidogo katika kuyatekeleza.