Mjumbe wa China atoa mwito wa kuondoa vikwazo dhidi ya Sudan
2022-03-29 09:00:17| CRI

Naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing, jana alitoa mwito wa kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Sudan.

Akiongea kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Balozi Dai amesema kufuatia kuondoka kwa tume ya pamoja kulinda amani ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika jimbo la Darfur, na Sudan  imebeba wajibu mkuu wa kuwalinda raia, kuna haja ya kuimarisha haraka uwezo wake wa kulinda usalama.

Kwa mujibu wa azimio nambari 2620 lililopitishwa na Baraza la Usalama mwezi uliopita, inatakiwa kuwe na maendeleo kabla ya Agosti 31 mwaka huu ili kurekebisha kigezo cha kuwekea vikwazo hivyo. Balozi Dai amesema China inatarajia kuwa hitaji hilo linaweza kutimizwa kwa ufanisi, na ametoa mwito wa kuzitaka nchi husika zibadilishe mwelekeo, zijitahidi kutendeana kwa usawa na kushirikiana ili kupata maendeleo kwa pamoja.