Rais wa Ghana azindua mradi wa mawasiliano uliojengwa na kampuni ya China
2022-03-30 09:11:35| CRI

Rais Nana Addo Dankwa Akufo-Addo wa Ghana amezindua mradi wa barabara ya makutano uliojengwa na kampuni ya China mjini Tamale.

Mradi huo uliojengwa na kampuni ya Sinohydro ukiwa na daraja kuu lenye urefu wa mita 684, unatarajiwa kuboresha kwa kiasi kikubwa hali ya mawasiliano katikati ya mji.

Rais Akufo-Addo amepongeza mradi huo kutoa nafasi kubwa ya mjini kwa manufaa ya watu wa Ghana, huku akisema mradi huo ni mfano mzuri wa uhusiano mzuri kati ya Ghana na China.

Balozi wa China nchini Ghana Bw. Lu Kun ameipongeza kampuni ya China kutokana na juhudi zake katika miaka mitatu iliyopita wakati ikikabiliana na changamoto zilizotokana na COVID-19.

Ujenzi wa mradi huo ulianza mwezi Aprili mwaka 2019, ambao ni mradi mkuu katika makubaliano ya uungaji mkono wa miradi mikubwa yaliyosainiwa kati ya serikali ya Ghana na kampuni ya China.