Mchumi asema ushirikiano kati ya Namibia na China unaimarika
2022-03-30 09:12:27| CRI

Mchumi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Namibia Bw. Lameck Odada, amesema uhusiano wa jadi kati ya Namibia na China umeimarika katika miaka iliyopita, ukibadilika kuwa ushirikiano wa kimkakati unaoleta mafanikio.

Bw. Odada amesema katika miaka kadhaa iliyopita nchi hizo mbili zimejenga uhusiano imara kupitia ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, maendeleo ya miundombinu, kilimo, michezo, biashara na afya.

Amesema mchango wa China katika maendeleo ya miradi mikuu ya miundombinu ikiwemo bandari ya Walvis Bay, miundombinu ya barabara, uboreshaji wa viwanja vya ndege, reli na barabara kuu, umeimarisha na kuinua hadhi ya kimkakati ya Namibia katika ushindani wa biashara wa kikanda na kibara.