Ethiopia yapata dola milioni 24 za kimarekani kutokana na eneo la viwanda lililojengwa China
2022-03-30 08:42:58| CRI

Ethiopia imepata mapato ya dola za kimarekani milioni 24 kutokana na eneo la viwanda lililojengwa na China kwenye miezi sita ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/22 ulioanza Julai 8.

Maneja mkuu wa eneo la viwanda la Debre-Birhan Bw. Yeshitila Mulugeta amesema mapato hayo yametokana na bidhaa za kilimo na nguo zilizozalishwa katika kipindi hicho.

Eneo la viwanda la Debre-Birhan lililoko kilomita 110 kaskazini mwa Addis Ababa, lilijengwa na kampuni ya ujenzi wa mawasiliano ya China (CCCC), na lilizinduliwa rasmi mwezi Machi mwaka 2019. Mpaka sasa imetoa nafasi 1,700 za ajira kwa raia wa Ethiopia.