Rais wa Tunisia avunja bunge baada ya kusitishwa kwa miezi minane
2022-03-31 08:59:44| CRI

Rais Kais Saied wa Tunisia ametangaza kuvunja bunge la nchi hiyo alipohutubia taifa kupitia televisheni ya Wataniya 1.

Kwenye hotuba yake, rais Saied amesema nchi hiyo inakabiliwa na jaribio la mapinduzi, na jukumu lake ni kulinda nchi, taasisi zake na watu wake.

Rais Saied ameonya dhidi ya jaribio lolote la kuchochea machafuko na mgawanyo wa ndani. Tarehe 25 Julai mwaka jana rais Saied alimfuta kazi aliyekuwa waziri mkuu Hichem Mechich na kusitisha shughuli zote za bunge.