Waziri wa mambo ya nje wa China afanya mazungumzo na wenzake wa Pakistan na Russia
2022-03-31 09:23:26| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana huko Tunxi mkoani Anhui alifanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na mwenzake wa Pakistan Bw. Moeen Qureshi, na mwenzake wa Russia Bw. Sergey Lavrov waliohudhuria mkutano wa tatu wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi jirani za Afghanistan.

Bw. Wang Yi alipofanya mazungumzo na Bw. Qureshi alisema China itaendelea kuhimiza uhusiano kati ya China na Pakistan na kuiunga mkono Pakistan kulinda mamlaka ya nchi , ukamilifu wa ardhi, heshima ya taifa, na China itaendelea kuwa rafiki wa kuaminika  kwa Pakistan.

Alipofanya mazungumzo na Bw. Lavrov, Bw. Wang Yi alisema China inapenda kushirikiana na Russia kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizi mbili kwenye msingi wa makubaliano yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili. Kuhusu suala la Ukraine Bw. Wang alisema China inaunga mkono kuendelea na mazungumzo ya amani kati ya Russia na Ukraine na kuunga mkono juhudi za Russia na pande mbalimbali za kuzuia msukosuko wa kibinadamu.