Rais Xi Jinping wa China jana alishiriki kwenye shughuli ya upandaji miti iliyofanyika hapa Beijing, shughuli ambayo ameshiriki kwa miaka 10 mfululizo.
Akiongea kwenye shughuli hiyo, Rais Xi alisema anapenda kuchangia juhudi zake kwenye harakati ya kuifanya China iwe ya kupendeza, kupanda mbegu ya uhifadhi wa mazingira ya asili katika jamii nzima, na hasa miongoni mwa vijana.
Rais Xi pia amesema kutokana na juhudi endelevu, wataweza kuifanya China iwe na anga ya bluu zaidi, milima ya kijani zaidi, maji safi zaidi na mazingira ya kupendeza zaidi.
Rais Xi aliambatana na viongozi wengine waandamizi wa chama na serikali, ambao walijumuika na watu kadhaa wanaojitolea kupanda miti kwenye bustani yenye eneo la hekta 100 lililoko kusini mwa mji wa Beijing.