Mashindano ya Worldskills Africa yahimiza ujenzi wa uwezo kwa vijana
2022-03-31 09:00:15| CRI

Makala ya pili ya mashindano ya Worldskills Africa, inayoendelea huko Swakopmund, Namibia, inahimiza maendeleo ya uwezo miongoni mwa vijana wa Afrika.

Mashindano hayo ya mwaka huu yanafuatilia ushirikiano kati ya wataalamu wa kimataifa na wa ndani wa WorldSkills kwenye utoaji wa mafunzo, na kuhimiza mbinu za usanifu shirikishi.

Mhandisi wa ndege na matengenezo kutoka Zambia Bi. Euphrasia Mulenga, aliyeshiriki kwa mara ya pili, amesema mashindano hayo yanaweka jukwaa kwa vijana kuonesha uwezo na ustadi wao.

Vijana zaidi ya 100 kutoka nchi 11 za Afrika wanashiriki katika mashindano hayo yanayohusisha maeneo 16 tofauti ya kiufundi na kiustadi.