Televisheni ya StarTimes na kampuni ya Bboxx kushirikiana kutoa huduma ya televisheni nchini Kenya
2022-03-31 08:56:02| CRI

Kampuni ya televisheni ya kulipia ya China StarTimes nchini Kenya imetangaza kushirikiana na kampuni ya huduma ya umeme wa nishati ya jua Bboxx, ili kuwawezesha wateja wasio na huduma ya umeme kutazama televisheni.

Ushirikiano huo unatoa fursa kwa wateja wasio na umeme kununua mfumo wa umeme wa nishati ya jua pamoja na seti moja ya televisheni yenye antena au dishi la StarTimes, ili waweze kupata matangazo ya chaneli za ndani na kimataifa.

Mkuu wa kampuni ya StarTimes tawi la Kenya Bw. Hanson Wang, amesema ushirikiano huu utatoa mchango mkubwa katika kuwawezesha watu kupata manufaa ya kijamii kupitia habari na burudani kuwafikia nyumbani.