China kuwawekea vizuizi vya visa kwa baadhi ya maofisa husika wa Marekani
2022-04-01 08:44:59| CRI

China imeamua kuweka vizuizi vya visa dhidi ya baadhi ya maofisa wa Marekani waliotunga uongo kuhusu masuala ya haki za binadamu nchini China, kuhimiza vikwazo dhidi ya China na kuhujumu maslahi ya China.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin alitangaza uamuzi huo baada ya Marekani kutangaza kuwawekea vizuizi vya visa maofisa wa China kutokana na kile wanachokiitia “ukiukaji wa haki za binadamu”.

Bw. Wang amesema Marekani ilitunga uongo wa kiovu kuhusu masuala ya haki za binadamu na kuutumia kama kisingizio cha kuingilia mambo ya ndani ya China, kuharibu sifa ya China na kuwakandamiza maofisa wa China, vitendo ambavyo vimekiuka vibaya sheria ya kimataifa na kanuni za kawaida kwenye mahusiano ya kimataifa.