Tatizo la Usonji kwa Watoto
2022-04-01 08:23:12| CRI

Tarehe 2 Aprili ni Siku ya Kimataifa ya Usonji. Tatizo la Usonji ambalo bado utafiti unaendelea kufahamu chanzo chake, limeendelea kuongezeka siku hadi siku, na hii inatokana na uelewa mdogo wa jamii kuhusu tatizo hilo. Watoto wanapogunduliwa mapema kuwa na usonji, wanaweza kupewa huduma stahiki na hivyo kuwasaidia kushinda changamoto zinazotokana na hali hiyo. Katika kipindi hiki tunazungumzia tatizo hili la usonji kwa watoto, na jinsi ya kukabiliana nalo.